Masharti ya Matumizi
Sehemu ya tovuti hii imetayarishwa ili kukusaidia ujifunze mengi zaidi kuhusu masuala ya fedha, mifumo ya kibenki, mikopo, vyama vya ushirika, n.k. Soma, tazama, na pakua elimu inayokupendeza.
413,961 already enrolled!
Tungependa wengine pia wanufaike na tovuti hii, lakini tafadhali usitumie habari zilizomo kutengeneza tovuti au programu nyingine. Unaweza kushirikisha na wengine mambo uliyojifunza kwa kuwaelekeza kwenye tovuti hii kulingana na Masharti ya Utumiaji yafuatayo.
- Haki ya Kunakili
- Alama za Usajili
- Masharti ya Utumiaji na Leseni ya Kutumia Tovuti Hii
- Sehemu ya Kifedha
- Hati ya Kukataa Kubadilisha au Kurekebisha Bidhaa na Kutowajibika Kisheria
- Kuvunja Masharti ya Utumiaji

Alan Minkys
Instructor in Marketing
- 20 hours on-demand video
- Full Lifetime Access
- Access on Mobile and TV
- Certificate of Completion
Haki ya Kunakili
© 2023 Starter Saving And Capital Fund (SSCF) – Dar es Salaam. Haki zote zimehifadhiwa.
Tovuti hii imetayarishwa na inasimamiwa na SSCF. Isipokuwa iwe imeonyeshwa vinginevyo, habari zote zilizo katika tovuti hii ni mali ya SSCF.

Alama za Usajili
Jina Adobe, nembo ya Adobe, Jina Acrobat, na nembo ya Acrobat ni nembo za Adobe Systems Incorporated. iTunes na iPod ni nembo za Apple Inc. Jina Microsoft, nembo ya Microsoft, pamoja na majina ya programu yoyote ya Microsoft na bidhaa zake kama vile Microsoft Office na Microsoft Office 365 ni alama za usajili za Microsoft Inc. Android ni alama ya usajili ya Google LLC. Roboti ya android imetokezwa na kuboreshwa kupitia kazi iliyofanywa na kusambazwa na Google na kutumiwa kulingana na masharti yaliyowekwa katika leseni ya Creative Commons 3.0 Attribution License (https://creativecommons.org/licenses/by/3.0/us/). Alama nyingine zote na nembo zilizosajiliwa ni mali ya wanaozimiliki.
Masharti ya Utumiaji Tovuti Hii
Masharti ya Utumiaji yanaongoza jinsi tovuti hii itakavyotumiwa. Unapotumia tovuti hii, unakubaliana kikamili na Masharti ya Utumiaji, pamoja na masharti yoyote ya utumiaji yaliyoongezwa (“Masharti ya Utumiaji” kwa ujumla) yaliyowekwa kwenye tovuti hii. Ikiwa hukubaliani na Masharti ya Utumiaji au sehemu yoyote ya Masharti hayo, hupaswi kutumia tovuti hii.
Ni mambo gani yanayoonyesha unaitumia vizuri? Kufuatana na vizuizi vilivyoorodheshwa hapa chini, unaweza kufanya yafuatayo:
Unaweza kutazama, kupakua, na kuchapisha picha, machapisho ya kielektroni, muziki, maandishi, au video zilizo na haki ya kunakili kutoka katika tovuti hii kwa ajili ya matumizi yako yasiyo ya kibiashara.
Kushiriki na wengine viunganishi (links) au nakala za machapisho ya kielektroni, video, au programu za sauti ulizopakua kutoka katika tovuti hii.
Hupaswi:
Kupachika picha, machapisho ya kielektroni, muziki, maandishi, video, nembo au alama za usajili, au makala kwenye Intaneti kutoka kwenye tovuti hii (iwe ni katika tovuti, kituo cha kushiriki faili au video, au mtandao wa kijamii).
Kusambaza picha, machapisho ya kielektroni, muziki, maandishi, video, nembo au alama za usajili kutoka kwenye tovuti zikiwa sehemu ya au pamoja na programu yoyote ya kompyuta (kutia ndani kupakia habari hizi katika server kwa matumizi ya programu fulani ya kompyuta).
Kufanyiza upya, kunakili, kusambaza, au kutumia kwa njia isiyofaa picha zozote, machapisho ya kielektroni, muziki, maandishi, video, nembo au alama za usajili kutoka katika tovuti hii kwa matumizi ya kibiashara au kupata malipo (hata ikiwa hupati faida).
Kutengeneza programu za kompyuta, vifaa, au mbinu zenye kusudi la kukusanya, kunakili, kupakua, kupata (extract), kuvuna (harvest), au kutoa (scrape) habari (data), HTML, picha, au maandishi kutoka katika tovuti hii kwa kusudi la kusambaza. (Hii haitii ndani kusambaza programu za bure, zisizo za kibiashara zenye kusudi la kupakua faili za kielektoni kama vile, EPUB, PDF, MP3, AAC, MOBI, na faili za MP4 kutoka katika maeneo ya umma ya tovuti hii.)
Kutumia vibaya tovuti hii au huduma zake, kama vile kuvuruga au kuingia kwenye tovuti hii au huduma zake kupitia mbinu nyingine isipokuwa ile ambayo imeruhusiwa.
Kutumia tovuti hii kwa njia yoyote inayosababisha, au itakayosababisha madhara, au kuzuia isipatikane au wengine wasiweze kuitumia; au kwa njia yoyote ambayo ni kinyume na sheria, isiyo halali, ya ulaghai, au yenye kudhuru, au kwa njia yoyote inayohusisha kuvunja sheria, isiyo halali, ya ulaghai, au kwa kusudi au utendaji wenye madhara.
Kutumia tovuti hii au picha zozote, machapisho ya kielektroni, muziki, maandishi, video, nembo au alama za usajili kutoka katika tovuti hii kwa kusudi lolote linalohusiana na uuzaji.
Tovuti hii hutumia Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps), huduma inayopatikana kupitia mtu wa tatu ambayo hatuwezi kuisimamia. Utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) katika tovuti yetu unategemea masharti ya utumiaji ya ziada yanayotumika wakati huo Google Maps/Google Earth Additional Terms of Service. Hawatujulishi kuhusu usasishaji wa huduma zao, hivyo basi tafadhali pitia masharti ya utumiaji (Google Maps Service) kabla ya kutumia huduma hiyo. Usitumie Huduma ya Ramani ya Google ikiwa haukubaliani na masharti ya utumiaji. Huduma ya Ramani ya Google haitoturudishia habari zinazohusu utumiaji wako.
Sehemu ya Blogu
Habari zilizomo katika sehemu ya blogu ya tovuti hii (“Sehemu ya Blogu”) ni kwa kusudi la kuelimisha na si kutoa ushauri wa kifedha, na wala si kwa kusudi la kuchukua mahala pa ushauri wa kitaalamu, uchunguzi au fedha. Sehemu hii ya Blogu haipendekezi hatua zozote za kuchukua, kihasibu, bidhaa, maoni, au habari nyingine zozote zitakazopatikana katika Sehemu hii ya Blogu.
Mara zote wasiliana na mtaalam wa fedha anayestahili ikiwa una maswali yoyote kuhusu mtanziko wa kifedha au hatua fulani.
Jitihada imefanywa ili Sehemu hii ya Blogu katika tovuti yetu iwe na habari zilizo sahihi na za hivi karibuni. Hata hivyo, habari zinazopatikana katika Sehemu hii ya Blogu zinatolewa bila uhakikisho (“AS IS” without warranty), wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja.
Tovuti hii haitawajibika kwa habari zinazopatikana katika Sehemu ya Blogu kutia ndani kutobeba lawama kwa matarajio ya kufaa kwa matumizi ya habari zinazopatikana.
Tovuti hii haitoi uhakikisho wa kutegemeka, kufaa, usahihi, na ukamili wa habari hizo au ikiwa habari zinazopatikana katika Sehemu ya Blogu ni za karibuni zaidi. Tovuti hii haitabeba lawama au kuwajibika kwa makosa yoyote au mapungufu katika habari zinazopatika kwenye Sehemu ya Blogu. Hatuwajibiki ikiwa utaamua kutumia habari zozote zilizo katika Sehemu hii ya Blogu. Hatuwajibiki kwa madai au madhara yoyote (kutia ndani, madhara endelevu (without limitation), madhara madogo yanayojitokeza (incidental) na makubwa (consequential), faida zitakazopotezwa, au madhara yanayotokana na habari (data) zilizopotea au kukatishwa kwa biashara) yatakayosababishwa na kutumiwa au kushindwa kutumiwa vizuri kwa Sehemu ya Blogu; haijarishi ikiwa madai au madhara hayo yanategemea uhakikisho (warranty), mkataba, kosa (tort), au dhana yoyote nyingine ya kisheria, hata ikiwa tovuti hii inajulishwa au la kuhusu uwezekano wa madai au madhara hayo.
Hati ya Kukataa Kubadilisha au Kurekebisha Bidhaa na Kutowajibika Kisheria
Tovuti hii na taarifa zote, mambo yaliyomo, vitu vilivyomo na huduma nyingine unazopata kupitia tovuti, zinatolewa na SSCF “kama zilivyo.” SSCF haitoi uwakilishi au hati ya kubadili au kurekebisha bidhaa ya aina yoyote, kwa njia ya waziwazi au isiyo ya waziwazi.
SSCF haitoi uhakikisho kwamba tovuti hii haina virusi au mambo mengine yasiyofaa. SSCF haitahusika na madhara ya aina yoyote yanayotokana na kutumia huduma yoyote, au kutokana na taarifa yoyote, mambo yoyote yaliyomo, vitu vyovyote vilivyomo au huduma yoyote unayopata kupitia tovuti, kutia ndani, kutowajibika kwa madhara ya moja kwa moja, yasiyo ya moja kwa moja, yanayoweza kutokea, adhabu, na hasara inayotokea (kutia ndani kutopata faida).
Kuvunja Masharti ya Utumiaji
Kupatana na haki nyingine za SSCF zilizo chini ya Masharti haya ya Utumiaji, ukivunja Masharti haya ya Utumiaji kwa njia yoyote, SSCF inaweza kuchukua hatua kwa njia yoyote inayoona kuwa inafaa ili kukabiliana na uvunjaji huo wa masharti haya, kutia ndani kukuzuia kwa muda usiingie kwenye tovuti hii, kukuzuia kabisa usiingie kwenye tovuti hii, kuzuia kompyuta zinazotumia anwani yako ya IP zisiingie kwenye tovuti yetu, kuwasiliana na kampuni inayokuandalia huduma za Intaneti na kuiomba izuie usiweze kuingia kwenye tovuti hii na/au kukuchukulia hatua ya kisheria.
Marekebisho
SSCF inaweza kurekebisha haya Masharti ya Utumiaji wakati wowote. Masharti ya Utumiaji yaliyorekebishwa ya Tovuti hii yatatumika kuanzia tarehe ambayo Masharti hayo yaliyorekebishwa ya Utumiaji yatakapochapishwa katika Tovuti hii. Tafadhali angalia ukurasa huu kwa ukawaida ili kuhakikisha unafahamu vizuri masharti ya karibuni zaidi.
Sheria na Eneo
Masharti haya ya Utumiaji yataongozwa na sheria za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, bila kujali iwapo zinahitilafiana na sheria nyingine. Hatua yoyote ya kisheria itakayochukuliwa kuhusiana na Masharti haya ya Utumiaji itashughulikiwa katika mahakama iliyo chini ya usimamizi wa Jamuhuri.
Uzuiaji
Iwapo mahakama yoyote inayostahili itaamua kwamba sehemu moja ya Masharti haya ya Utumiaji ni batili, haifai, haiwezi kutekelezwa, au haipatani na sheria, masharti mengine bado yataendelea kutumika. Kushindwa kwa SSCF kuhakikisha kwamba sehemu moja ya Masharti haya ya Utumiaji inafuatwa hakumaanishi wala hakupaswi kufikiriwa kuwa eti kifungu fulani kimefutiliwa mbali au eti haki ya kukitekeleza imeondolewa.
Mkataba Wote
Masharti haya ya Utumiaji ndio mkataba wote kati yako na SSCF unapotumia tovuti hii, na mkataba huu unachukua mahali pa mikataba mingine yote uliyowahi kufanya kuhusiana na utumiaji wa tovuti hii.