MBINU 6 Unazoweza Kutumia Kujenga Mfuko wa Dharura

Kwa namna moja ama nyingine, sote tumekumbwa na hali ya dharura ya kifedha — mathalani gharama za matibabu, kifaa au mashine za kazi kuharibika, hasara katika baiashara, au kupoteza simu. Haijalishi dharura ni kubwa au ndogo, gharama hizi zisizotarajiwa mara nyingi huja katika wakati mgumu na mara nyingi kwa kuambatana.

Kuweka akiba maalum kwa ajili ya dharua au mfuko wa dharura ni njia moja muhimu ya kujilinda, na inaweza kukupa utulivu wa fikra na kukuongezea nafasi kubwa zaidi ya kufikia malengo yako makubwa katika siku za usoni.

Kwa sababu hiyo, wote tunakubalina kwamba kuwa na mfuko wa dharura ni mojawapo ya malengo muhimu kuwa nayo. Swali ni Je, wewe unatumia mikakati gani kuhakikisha kuwa akiba yako ya dharura hauitumii ili ije ikufae wakati wa dharura ya kweli? Na Je, una mahali maalum unapoihifadhi akiba hiyo?

Katika makala haya tutaangazia juu ya mfuko wa dharura na kukusaidia kujibu baadhi maswali ambayo pengine umekuwa ukijiuliza mara kwa mara pasina mjibu… maswali kama:

  • Mfuko wa dharura ni nini?
  • Kwa nini ninauhitaji?
  • Je, ninahitaji kiasi kuweka kiasi gani?
  • Je, nitaujengaje?
  • Nitunze wapi pesa zangu?
  • Ninapaswa kuzitumia lini?

Mfuko wa Dharura ni Nini?

Mfuko wa dharura ni akiba ya pesa ambayo imetengwa mahsusi kwa ajili ya mahitaji ya dharura ya kifedha. Baadhi ya mifano ya kawaida ni pamoja na ukarabati wa gari, ukarabati wa nyumba, bili za matibabu, au hasara kataka biashara, n.k.

Kwa ujumla, mfuko wa dharura unaweza kutumika kulipia bili kubwa au ndogo ambazo hazijapangwa au malipo ambayo si sehemu ya gharama na matumizi yako ya kila mwezi.

Kwa Nini Ninauhitaji?

Bila kuwa na mfuko wa dharura, mtikisiko wa kifedha (kiuchumi) —hata kama ni mdogo—unaweza kukurudisha nyuma, na usipokuwa makini, unaweza kukusababishia matokeo hasi na wakati mwingine ya kudumu.

Utafiti unaonyesha kwamba watu ambao wanaopata madhira makubwa kutokana na mtikisiko wa kifedha ni wale ambao hawakuwa na akiba kabisa au walikuwa na akiba kidogo ya kusaidia kuwalinda dhidi ya dharura kwa siku zijazo. Wanaishia kutegemea mikopo, na zaidi kwenye mikopo humiza ambayo inawaacha na makovu.

Je, Ninahitaji Kuweka Akiba Kiasi Gani Ndani ya Mfuko?

Kiasi unachohitaji kuwa nacho katika mfuko wa dharura kinaamuliwa na hali yako ya kifedha pamoja na kiu uliyo nayo. Fikiria juu ya aina ya gharama za kawaida zisizotarajiwa ambazo umeshakuwa nazo hapo awali na zilikuwa kiasi gani. Hii itakusaidia kuweka lengo la ni kiasi gani ungependa kukitenga.

Ikiwa unaishi kwa malipo ya siku au mapato yako hayalingani kwa wiki au mwezi, pengine unaweza kuhisi ni vigumu kuweka akiba. Lakini, hata ukiamua kuweka akiba ya kiasi kidogo, kidogo… kiasi hicho kinaweza kukupa unafuu fulani wa kifedha.

Endelea kusoma ili kupata mbinu ya kuweka akiba, au mikakati inayokufaa zaidi.

Je, Nitaujengaje?

Kuna mbinu tofauti za kuanza kutia hela kwenye mfuko wa dharura. Hapa chini tumekupendekezea baadhi ya MBINU ambazo endapo ukiamua kuzifanyia kazi, ni matumaini yetu kwamba zitakuwa za msaada mkubwa kwako. Hata hivyo, mbinu hizi utegemeana na hali ya kifedha ya muhusika. Huenda ukatumia mbinu hizi zote, lakini hata kama una uwezo mdogo kifedha… kudhibiti matumizi yako na kuweka sehemu ya mapato yako ndiyo msingi mkuu na wa kuanzia.

Hebu tuanze kuangazia mbinu hizi 6 ambazo unaweza kuzitumia kujenga mfuko wa dharura.

MBINU 1: Jenga Tabia ya Kuweka Akiba

Kuweka akiba ya kiwango chochote kiwe -kikubwa au kidogo- ni rahisi endapo utajenga utamaduni wa kuweka akiba kila wakati. Ni mojawapo ya njia za haraka sana za kuona akiba ikiongezeka. Ikiwa huna tabia ya kuweka akiba, hapa chini nimekuorodheshea kanuni chache muhimu za kuzingatia ili kuweza kujenga tabia ya kuweka akiba:

Weka lengo la kufanikisha jambo linalokunyima usingizi. Kuwa na lengo mahususi la kuweka akiba na hatimaye kufanikisha jambo linankunyima usingizi, kunaweza kukusaidia kukupa hamasa. Kuanzisha mfuko wa dharura kunahitaji uwe na lengo linaloweza kufikiwa na zaidi ambalo linakunyima usingizi, haswa unapoanza. Mathalani, wewe ni mtu mzima ambaye bado unaishi nyumbani kwenu kwa sababu huna uwezo wa kupanga nyumba. Na jambo hili linakukera na kukunyima usingizi 😒
Hili linaweza kuwa lengo chechemuzi la kukufanya uanze kujenga tabia ya kuweka akiba.

Unaweza kutumia kikokotoo chetu kubaini itakuchukua muda gani kufikia lengo lako, kulingana na kiasi na mara ngapi unaweza kuweka pesa.

Unda mfumo thabiti wa kutoa michango. Kuna idadi ya njia tofauti za kuweka akiba, na kama utakavyosoma hapa chini, kusanidi uhamishaji wa fedha kwa njia ya kielektroniki mara kwa mara ndio njia rahisi zaidi. Huenda pia ukaweka kando kiasi maalum cha pesa kila siku, wiki au siku ya kupokea malipo. Hakikisha unajilipa kwanza kwa kuweka hela kwenye mfuko wa dharura.

Fuatilia maendeleo ya mfuko wako mara kwa mara. Tafuta njia ya kuangalia akiba yako mara kwa mara. Iwe ni kwa kuangalia salio la akaunti yako au kuandika jumla inayoendelea ya michango yako, kutafuta njia ya kutazama maendeleo yako kunaweza kukupa furaha na kukutia moyo kuendelea.

Sherehekea mafanikio yako. Ikiwa unaona unaendelea vizuri na utaratibu uliojiwekea wa kuweka akiba, basi usikose kupata wasaa mzuri wa kutambua, kujipongeza na kusherekea kile ambacho umetimiza. Angalizo: Usitumie fedha nyingi kujipongeza 😂

Je, hii inamfaa nani: Mtu yeyote, lakini hasa wale walio na mapato ya kuhaminika.

MBINU 2: Simamia Mtiririko Wako wa Pesa

Mtiririko wa pesa kimsingi ni pale pesa zako zinapoingia (mapato yako) na kutoka (gharama na matumizi yako). Ikiwa una utaratibu wa kufuatilia kikamilifu, utaanza kuona ni wapi pa kurekebisha ili uweze kupata hela ya ziada ya kuweka kwenye mfuko wa akiba.

Je, hii inamfaa nani: Mtu yeyote. Hii ni hatua moja muhimu ya kwanza katika kudhibiti matumizi mabaya ya pesa zako, bila kujali kama unaishi kwa mshahara au biashara.

MBINU 3: Tumia Kipato cha Mara Moja Kuweka Akiba

Kunaweza pia kuwa na nyakati fulani katika mwaka unapopata kiwango kikubwa cha pesa. Mfano umepata hela ya likizo, uhamisho,  zawadi ya siku ya kuzaliwa, n.k.

Ingawa inavutia kuzitumia, kuokoa pesa zote au sehemu ya pesa hizo kunaweza kukusaidia kuanzisha mfuko wako wa dharura haraka.

Je, hii inamfaa nani: Mtu yeyote lakini hasa wale walio na mapato yasiyo rasmi. 

MBINU 4: Tumia Miamala ya Kielektroniki

Kuweka akiba kwa njia ya kielekroniki ni mojawapo ya njia rahisi zaidi kutunisha mfuko wako wa dharura. Njia moja ya kawaida ya kufanya hivyo ni kuiambia benki ihamishe pesa kiotomatiki kwenda kwenye akaunti yako ya mfuko wa dharura. Unaweza kuamua ni kiasi gani na mara ngapi kwa mwezi.

Ni wazo nzuri kuzingatia mizani yako ya kipato, hata hivyo, ili usiingie kwenye tozo za ziada. 

Je, hii inamfaa nani: Mtu yeyote, lakini hasa wale walio na kipato cha kuhaminika. 

MBINU 5: Hifadhi Kupitia Mwajiri Wako

Njia nyingine ya kuweka akiba kwenye mfuko wa dharura ni kupitia mwajiri wako. Mbali na michango inayotemgemea mwajiri kwa ajili ya mifuko ya hifadhi ya jamii, unaweza kuamua kupeleka kiwango fulani katika mfuko wa dharura. Hii ni njia rahisi ikiwa unapata majaribu ya kutaka kutumia fedha yako kila unapoipata.

Je, hii inamfaa nani: Mtu yeyote, lakini hasa wale walioajiriwa. 

Niweke Wapi Pesa Zangu?

Mahali unapoweka pesa za mfuko wako wa dharura inategemeana na uchaguzi wako. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa ziko salama, zinapatikana, na katika mahali ambapo hutashawishika kuzitumia kwa mambo yasiyo ya dharura.

Hapa tuna mapendekezo machache ya mahali pa kuweka akiba yako ya dharura… unaweza kuchagua ile inayokufaa zaidi:

Akaunti ya benki — Fungua akaunti maalum yaan fixed account katika benki ambayo unadhani kuwa ni mojawapo ya benki salama zaidi ya kuweka pesa zako. 

Kwenye Kadi ya Simu — Mitandao mingi ya simu inatoa huduma za kifedha, mfano M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, EzyPesa, n.k. Kadi hizi haijaunganishwa na benki na hivyo unaweza kutumia tu kiasi kilicho kwenye kadi yako.

Kibubu — Chaguo jingine ni kuweka pesa kwenye kibubu kwa ajili ya dharura, iwe nyumbani kwako au kwa mwanafamilia au rafiki unayemwamini. Kumbuka kwamba pesa zinaweza kuibiwa, kupotea au kuharibiwa.   

Ni Wakati Gani Ninapaswa Kuutumia?

Jiwekee baadhi ya miongozo juu ya kile kinachojumuisha gharama ya dharura na isyo ya dharura. Sio kila gharama zisizotarajiwa ni dharura hivyo unahitaji kuwa makini. 

Kuwa na mfuko wa dharura kunaweza kukusaidia kuepuka kutegemea aina nyingine za mikopo isiyo ya lazima au mikopo umiza. 

Walakini, usiogope kuitumia ikiwa kweli unahitaji. Ikiwa unatumia chini kile kilicho katika mfuko wako wa dharura, ongeza bidii ili uimarishe tena. Kujizoeza ustadi wako wa kuweka akiba kwa muda kutarahisisha hili.

Lusabara

Lusabara

Mwandishi wa makala hii ni mwanafunzi nje ya darasa. Mfikirivu, anayependa kutizama mambo kama yalivyo. Ni teja wa teknolojia na mwanafunzi wa masoko ya kidijitali na usanifu mifumo ya kyomputa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Let's make a difference together

We’re not here to just make a profit, we’re here to create a better world. We’re here to challenge the status quo and disrupt industries. We’re here to empower people and help them achieve their full potential. We’re here to have fun and enjoy the ride. Our mission is to make a positive impact by investing in and supporting innovative and passionate entrepreneurs who share our values. We’re not afraid to take risks and push boundaries, and we believe that by doing so, we can change the world for the better

Recent Posts

Follow Us

Join the thousands on the waitlist and help us reimagine banking for the people.

Grow your audience, chat, follow, like and comment with your friends on the platform. With an ever growing community of hustlers, there’s enough people to connect with and make new friends.