MUHIMU: KWA KUTUMIA TOVUTI YETU AU KUTUPATIA HABARI ZAKO ZA KIBINAFSI, UMEKUBALI KWAMBA HABARI ZOTE ZA KIBINAFSI ULIZOTUMA ZINAWEZA KUTUMIWA KWA NJIA NZURI NA KWA MAKUSUDI YALIYOELEZWA KWENYE SERA YA FARAGHA INAYOFUATA KULINGANA NA SHERIA NA TARATIBU ZA HABARI ZA KIBINAFSI.

KUHESHIMU FARAGHA YAKO

Tuna wajibu wa kulinda na kuheshimu faragha yako. Sera hii inaonyesha msingi wa kutumia taarifa zozote za kibinafsi tunazochukua kutoka kwako au zile unazotupatia katika tovuti yetu. Tunahifadhi baadhi ya taarifa za msingi unapotembelea tovuti yetu na tunatambua umuhimu wa kulinda usalama wa taarifa hizo na kukujulisha tutazifanyia nini. Unaweza kuamua kutupatia taarifa zile unazoona kuwa ni taarifa za kibinafsi. Neno “taarifa za kibinafsi” linalotumiwa katika sera hii linarejelea taarifa kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, anwani ya posta, namba ya simu, au taarifa nyingine yoyote ambayo inaweza kutumiwa kukutambulisha. Huhitaji kuweka taarifa zako za kibinafsi ili kutumia maeneo ya umma ya tovuti hii. Neno “tovuti” linatia ndani tovuti hii na nyingine zinazohusiana na hii.

WANAODHIBITI TAARIFA ZAKO

Tovuti hii ni mali ya Starter Saving And Capital Fund (“SSCF”), ni ushiriki wa akiba na mikopo wenye makao makuu jijini Dar es Salaam linalotegemeza utendaji wa wanachama na elimu ya kifedha. Ikiwa umeamua kwa hiari yako kufungua akaunti, kutoa mchango, kuomba kutembelewa, au kufanya jambo lolote ambalo linahitaji ueleze taarifa zako za kibinafsi, unaonyesha unakubaliana na Sera hii, pamoja na kukubali taarifa zako zihifadhiwe kwenye seva zilizoko Marekani na taarifa zako zikusanywe, zishughulikiwe, zihamishwe na kutunzwa na SSCF na mashirika mengine yanayohusiana nayo ambayo yanategemeza SSCF katika nchi mbalimbali kama zinavyohitajiwa ili kushughulikia ombi lako. Taasisi hiyo ya kifedha inafanya kazi ulimwenguni pote kupitia wabia mbalimbali wanaotambulika kisheria. Kwa kusudi la kulinda taarifa, sehemu nyingine zinazohusika zinatia ndani makutaniko, ofisi za tawi, na wabia wengine wanayohusiana na SSCF.

Wanaodhibiti taarifa zako za kibinafsi wanatofautiana ikitegemea kile unachohitaji katika tovuti. Kwa mfano, ikiwa unachangia shirika la kisheria katika nchi fulani, jina lako na taarifa zako za mawasiliano zitapelekwa kwenye taasisi hiyo ya kisheria kama ilivyoonyeshwa wakati ukituma mchango wako. Mfano mwingine, ikiwa unaomba kutembelewa, jina lako na taarifa zako za mawasiliano zitapelekwa kwenye ofisi ya tawi lililokaribu nawe ili kutimiza ombi lako.

Ili kukusaidia, ikiwa katika eneo unaloishi kuna sheria za kulinda taarifa za kibinafsi zinazotumika, unaweza kupata taarifa za mawasiliano kwa ajili ya eneo unaloishi katika ukurasa wa Watu Wanaolinda Taarifa.

 

USALAMA NA USIRI WA TAARIFA

Tunahakikisha kwamba taarifa zako za kibinafsi zipo salama. Tunatumia mfumo wa kisasa zaidi wa kuhifadhi taarifa na mbinu za usalama za kulinda taarifa zako za kibinafsi ili zisitumiwe bila ruhusa, zisitumiwe vibaya, zisibadilishwe bila ruhusa, zisiharibiwe kinyume cha sheria au zipotee bila kukusudia. Wote wanaoshughulikia taarifa zako za kibinafsi na mtu yeyote wa tatu anayehusika kushughulikia taarifa zako za kibinafsi wana wajibu wa kuheshimu usiri wa taarifa zako. Tunatunza taarifa zako za kibinafsi kwa muda zinapohitajika tu na kwa kusudi la kukusanywa au kwa kuzingatia ripoti yoyote ya kisheria inayohusika au matakwa ya kutunza taarifa yaliyoko kwenye hati.

Tunalinda taarifa zako za kibinafsi kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia, kama, teknolojia ya Transport Layer Security (TLS). Tunatumia mifumo ya kompyuta inayotumiwa na watu wachache inayotunzwa katika majengo yanayolindwa kielektroni, kwa kutumia watu na mikakati hususa iliyowekwa ili kulinda usiri na usalama wa taarifa za kibinafsi zinazotufikia. Tuna viwango imara vya usalama vinavyozuia matumizi yoyote ya taarifa bila kibali.

 

WATOTO

Ikiwa wewe ni mtoto kulingana na sheria za nchi na unatumia tovuti yetu, unaweza kutuma taarifa zako katika tovuti hii ikiwa tu ni kwa ajili ya uhamasishaji. Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi nawe umekubali mtoto atoe taarifa zake katika tovuti hii, unaonyesha umekubali Sera hii kwa ajili ya matumizi ya mtoto huyo.

 

TAARIFA KWA MTU WA TATU

Nyakati nyingine, tovuti itatumia viunganishi vinavyokuelekeza kwenye tovuti nyingine (third-party) itakayotoa huduma fulani kwa niaba yetu (kwa mfano, inapohusu kujaza fomu mtandaoni). Utatambua kwamba umeingia kwenye tovuti nyingine kwa sababu mwonekano wa tovuti hiyo utakuwa tofauti na anwani ya tovuti itabadilika. Kwa kuongezea, wanaweza kukutumia barua pepe au ujumbe kwenye simu yako kutokana na ombi ulilojaza katika tovuti hii na wanaweza kukujulisha kuhusu mambo ambayo ulikuwa unafanya kulingana na taarifa ulizojaza kupitia tovuti hii. Wakati tunapomchagua mtu wa tatu wa kutoa huduma, na mara kwa mara baada ya hapo, tunachunguza sera zao za faragha na za kulinda taarifa za kibinafsi ili kuhakikisha kwamba zina viwango vinavyofanana na vile tunavyotumia katika sera zetu. Hata hivyo, tovuti hizo nyingine hutoa program na huduma ambazo muundo wake, masharti ya utumiaji, sera za faragha, na mambo mengine yanayohusiana na utumiaji ambayo hatuwezi kudhibiti. Kwa sababu hiyo, utumiaji wako wa programu na huduma hizo ndani ya tovuti yetu utategemea masharti ya huduma yaliyopo wakati huo na matumizi ya tovuti hiyo kwa ujumla. Tovuti hizo zinaposasisha taarifa zao hazitujulishi, hivyo basi pitia masharti ya utumiaji kabla ya kutumia huduma zao. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera za tovuti hizo za kutoa huduma, tafadhali soma sera inayopatikana kwenye tovuti yao.

Utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) katika tovuti yetu unategemea sera ya faragha ya Google; Google Privacy Policy. Google ni mtu wa tatu ambaye programu, muundo na masharti yake; Terms of Service kwa ujumla yako nje ya uwezo wetu. Kwa hiyo, utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) uko chini ya Masharti Zaidi ya Huduma ya Ramani ya Google Google Maps/Google Earth Additional Terms of Service Hawatujulishi kuhusu usasishaji wa huduma zao, hivyo basi tafadhali pitia masharti ya utumiaji kabla ya kutumia huduma hiyo. Usitumie Huduma ya Ramani ya Google ikiwa hukubaliani na masharti ya utumiaji.

 

KUJULISHWA KUHUSU MABADILIKO YA SERA

 Tunaendelea kuboresha na kuongeza utendaji mpya na mambo mengine katika tovuti hii, na tunaboresha na kuongeza huduma nyingine. Kwa sababu ya mabadiliko yanayoendelea, pamoja na mabadiliko ya sheria na teknolojia, tunaweza kubadili jinsi tunavyotumia habari mara kwa mara. Tukihitaji kubadili Sera yetu, tutaonyesha mabadiliko hayo kwenye ukurasa huu ili sikuzote ujue habari tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia.

 

HATIJAVA (ACTIVE SCRIPTING AU JAVASCRIPT)

Hati hutumiwa na tovuti kuboresha utendaji wa tovuti. Kutumia ufundi wa hati huwezesha tovuti kurejesha habari zilizoombwa haraka zaidi kwa mtumiaji. Hati haitumiwi kamwe na tovuti kusakinisha programu kwenye kompyuta ya mtumiaji wala kukusanya habari kutoka kwa mtumiaji pasipo idhini.

Lazima HatiJava iwezeshwe katika kipekuzi ili sehemu fulani za tovuti zifanye kazi ifaavyo. Vivinjari vingi humruhusu mtumiaji kuwezesha au kulemaza hati hizo katika tovuti hususa. Soma habari kuhusu kipekuzi ili upate kujua jinsi ya kuwezesha hati katika tovuti teule.