Sera ya Faragha

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.

Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi

Sehemu nyingi za tovuti hii hazihitaji ujisajili wala kutuma habari zozote kwetu ili uzitumie. Hata hivyo, baadhi ya sehemu zinaweza kutumiwa na watumiaji waliojisajili, wale waliotuma maombi, au wale ambao taarifa zao za kibinafsi zimetumwa kwetu kutoka SSCF. Tutashughulikia taarifa zako za kibinafsi kulingana na vile ulivyokubali zitumiwe. Katika visa vingine, hata kama umevunja makubaliano, tunaweza kuwa na msingi halali wa kisheria wa kuendelea kushughulikia taarifa zako, ikiwa matakwa ya kisheria yanaturuhusu kufanya hivyo.

Taarifa za kibinafsi tunazopata kutoka kwako zilizoko kwenye tovuti yetu zinatumiwa kwa makusudi uliyoelezwa wakati ukijaza maombi. Makusudi hayo yanaweza kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:

Akaunti. Anwani ya barua-pepe au namba ya simu unayotumia unapofungua akaunti katika tovuti hii itatumiwa kuwasiliana nawe kuhusiana na akaunti yako. Kwa mfano, ukisahau jina lako la mtumiaji au nywila (nenosiri) yako na kuomba usaidiwe kuingia kwenye tovuti, utasaidiwa kupitia ujumbe utakaotumwa kwenye anwani ya barua-pepe uliyoingiza habari fupi kukuhusu.

Maombi. Ikiwa unakidhi vigezo kwa mujibu wa katiba ya chama pamoja na sera zake, unaweza kutumia tovuti hii kufungua akaunti ya kibinafsi, kutuma maombi, au mwakilishi wako anaweza kutumia tovuti hii kutuma maombi kwa niaba yako ikiwa utaona inafaa. Habari zako za kibinafsi zilizo katika akaunti yako zinaweza kutia ndani habari za kibinafsi ulizoandika, zilizoandikwa na wasimamizi wa mfumo, au mfanyakazi wa taasisi. Katika muktadha huo, taarifa hizo zitatumika tu kwa ajili ya kushughulikia na kuzingatia maombi yako na kwa madhumuni ya usimamizi, kutia ndani kuingiza maelezo yanayokuhusu yakiwa sehemu ya mchakato wa kushughulikia ombi. Ikihitajika, taarifa zako katika maombi zinaweza kupelekwa katika ofisi nyingine za tawi, makao makuu ya SSCF, au taasisi nyingine inayotumiwa na SSCF, mfano benki katika maeneo mbalimbali ili zishughulikiwe. Katika mchakato, kila ombi linashughulikiwa peke yake, na ili kuokoa muda, maombi mengi yatakuwa yakishughulikiwa kielektroniki.

Michango, Akiba, Uwekezaji, Uhamishaji. Unapotoa mchango wa pesa, kutuma salio, kuwekeza, kuweka akiba na hata kuomba mkopo, tunatumia taarifa zako kama zilivyo kwenye akaunti kuchakata na kukamilisha maombi yako. Miamala inayofanyika kupitia kadi za benki au simu za mkononi, hushughulikiwa na kampuni husika zinazotoa huduma za kuhamisha pesa mtandaoni na ambazo zina sera za ulinzi na usalama wa taarifa za kibinafsi zinazotambulika duniani pote. Tunaweza kupokea taarifa zako za kiuchumi, kama vile namba ya kadi ya benki au namba ya akaunti ya benki ili kushughulikia miamala yako, na kutuma habari zinazohitajiwa na wale wanaotoa huduma. Tunashughulikia muamala wako kwa njia salama ambazo zinapatana na viwango vya usalama wa taarifa za malipo  ujulikanao kama Payment Card Industry Data Security Standard. Baada ya muamala kukamilika, rekodi za miamala husika zitaifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiopungua miaka kumi. Rekodi hiyo inatia ndani rekodi ya tarehe ambayo muamala ulifanyika, salio, kiasi kilichotolewa, na njia iliyotumiwa. Hivyo, tunaenda sambamba na masharti ya uhasibu na kujibu maswali yoyote kutoka kwako kwa kipindi hicho. Taasisi inaweza kuwasiliana nawe muda wowote endapo italazimu kufanya hivyo.

Maombi ya Kupata Habari Zaidi au Kujifunza Kuhusu Taasisi. Unaweza pia kuomba habari zaidi au kujifunza SSCF na undani wa kazi zake kupitia tovuti yetu. Tutatumia tu habari za kibinafsi ulizotuma kwenye maombi yako kulingana na kile unachohitaji. Taarifa zako zinaweza kupelekwa kwenye ofisi nyingine za tawi au mashirika mengine yanayotumiwa na SSCF ikiwa ni muhimu kufanya hivyo ili kutekeleza maombi yako.

Makusudi Mengine. Unaweza kutuma taarifa zako za kibinafsi (kama vile jina, anwani ya posta, na namba ya simu) kwa ajili ya makusudi mengine tofauti na kufungua akaunti, kutuma maombi, au kufanya miamala. Katika kila kisa, kusudi la kuombwa utupatie taarifa fulani fulani zinakuwa wazi kabisa. Hatutatumia taarifa zako unazotupatia kwa ajili ya mambo ambayo huelezwi unapozitoa.

Tunakusanya, kuhifadhi, na kutumia taarifa za kibinafsi kwa ajili ya jambo unalohitaji tu, na tunazitunza taarifa hizo kwa muda tu ambao jambo hilo linashughulikiwa au kwa ajili ya makusudi mengine halali ya kutumia taarifa hizo. Katika hali hiyo, ikiwa utaamua kuficha baadhi ya taarifa za kibinafsi ambazo tumeziomba kutoka kwako, hutaweza kupata kibali cha kutumia sehemu fulani za huduma au hatutaweza kujibu maombi yako.

Taarifa unazotupatia katika maombi yako zinapelekwa kwa wale wanaohusika kuyashughulikia ili watimize kusudi la kutuma taarifa zako au kwa wataalamu wa ufundi wanaofanya kazi inayohusiana na kuendesha na kudumisha mfumo wa tovuti. Hatuwezi kumpa mtu yeyote taarifa zako za kibinafsi. Tutampa tu ikiwa (1) ni muhimu kufanya hivyo ili upate huduma uliyoomba na tutahakikisha unajua jambo hilo; (2) tunaamini kabisa kwamba kutoa taarifa hizo ni muhimu kutekeleza sheria au utaratibu unaotumika; (3) tunahitaji kuwajibu wenye mamlaka ya kusimamia sheria; au (4) inahitajika ili kutambua na kuzuia udanganyifu kwa ajili ya masuala ya kiusalama au kiufundi. Kwa kutumia tovuti hii, unakubali taarifa zako za kibinafsi zitolewe kwa mtu kwa ajili ya makusudi hayo pekee. Kwa hali yoyote ile, taarifa zozote za kibinafsi unazotupatia hazitauzwa, kufanyiwa biashara, au kukopeshwa.

 

KUTUMA TAARIFA NCHI NYINGINE

Taasisi hili ya kifedha inafanya kazi kote nchini Tanzania kupitia tovuti, simu janja, wakala na mashirika mbalimbali ya kifedha. Seva zinavyotoa huduma katika tovuti hii ziko Marekani. Kwa muktadha huo, tunutuma taarifa zako katika nchi nyingine, ambako sheria zao za kulinda taarifa ni tofauti kabisa na sheria za kulinda taarifa za nchi yetu. Tunaposhughulikia na kutuma taarifa zako za kibinafsi, tunachukua hatua madhubuti kulinda taarifa zako. Tunatarajia kwamba mashirika, makampuni yote yanayotumiwa na SSCF na yanayotegemeza kazi yao yafuate sera zetu za kulinda taarifa na sheria na taratibu hususa za taarifa za kibinafsi.

Kwa kutembelea tovuti hii na kuwasiliana nasi katika mtandao unaonyesha kwamba unakubali taarifa zako zitumwe kwenye nchi nyingine.

 

HAKI ZAKO

Wakati wowote unapotupa taarifa zako, tunachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba taarifa zako za ni sahihi na zinarekebishwa kwa ajili ya makusudi yaleyale yaliyofanya zikusanywe. Kwa kutegemea mazingira ya wakati huo, sheria za nchi zinazokubalika za kulinda taarifa, unaweza kuwa na haki zifuatazo kuhusiana na taarifa zako unazotutumia:

  • Unaweza kuomba taarifa kuhusu jinsi taarifa hizo za kibinafsi zinavyokusanywa na kutumiwa kulingana na sheria zinazokubalika katika nchi yetu;

  • Unaweza kuomba kuingia, kufunga, kufuta, au kurekebisha taarifa zako zako ikiwa hazijakamilika au si sahihi;

  • Ikiwa ni halali kisheria kufanya hivi, unaweza kuomba taarifa zako zisiendelee kufanyiwa kazi.

Unapotutumia maombi yako, wanaohusika katika kudhibiti taarifa watazingatia ombi lako kwa kulinganisha faida za mtu za kuweza kuingia kwenye taarifa zake au kuzirekebisha au kufuta taarifa zake na masilahi ya taasisi, kutia ndani labda ikiwa kukubaliwa kwa maombi hayo kunaweza kuhatarisha haki ya uhuru wako na shughuli nyinginezo. Pia, tutampa taarifa mtu yeyote wa tatu kuhusu mabadiliko yanayohitajika.

Tafadhali zingatia kwamba huenda taarifa zako zisiweze kufutwa ikiwa sheria inataka zishughulikiwe au ikiwa zinahitaji kutunzwa kwa misingi mingine ya kisheria. Kwa mfano, taasisi hii ya kifedha inaweka taarifa za kudumu za mtu zinazoonyesha kwamba yeye ni Mwanachama. Kufuta taarifa ya aina hiyo kutaingilia utendaji wa taasisi. Maombi ya kufuta taarifa zako yanategemea tutumiwe ripoti iliyotolewa mahakamani au hati inayoonyesha matakwa ya muda wa kutumia taarifa hizo. Pia, unaweza kupeleka malalamiko yako kwa wenye mamlaka ya kulinda taarifa kuhusu kutumiwa kwa taarifa ulizotupatia kupitia tovuti hii.