Sera ya SSCF ya Usalama wa Taarifa za Wanachama

Taasisi ya kifedha ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo la SSCF linaheshimu haki ya wanachama wake ya faragha na ya kulinda taarifa za kibinafsi. Ikiwa ni taasisi ya kifedha linatambua umuhimu wa mawasiliano ya wazi na ya kweli linapokusanya taarifa za kibinafsi na za siri ili kusimamia mahitaji ya wanachama inapotimiza utendaji na miamala ya kifedha, pamoja na kuhakikisha kwamba linadumisha siri na kuzilinda kabisa.

Taasisi mbalimbali kifedha kama ilivyo kwa SSCF, pamoja na sheria za nchi… zimepitisha sheria za kulinda taarifa ili kuhakikisha haki ya faragha ya kila mwanachama (mteja) inalindwa. Taasisi yetu pamoja na ofisi zake za tawi, sikuzote imekuwa ikiheshimu haki ya faragha na kudumisha siri, hata kabla ya kuundwa kwa sheria za kulinda taarifa. Taasisi hili ya kifedha itaendelea kulinda taarifa linazopokea kama ilivyo kawaida yake ya muda mrefu.

Kanuni za Kulinda Taarifa. Taasisi inatunza taarifa zote za wanachama kulingana na kanuni zifuatazo:

  1. Taarifa za mwanachama zitashughulikiwa kwa njia ya haki na ya kisheria.

  2. Taarifa za mwanachama zitakusanywa, kushughulikiwa, na kutumiwa kwa madhumuni ya kutimiza utendaji wa taasisi na kushughulikia miamala.

  3. Taarifa za mwanachama zitakuwa sahihi na ambazo hazijapitwa na wakati. Kosa lolote litasahihishwa mara tu linapogunduliwa na taasisi.

  4. Taarifa za mwanachama zitatunzwa na taasisi kwa kadiri zinavyohitajika ili zitumiwe kwa makusudi yanayofaa.

  5. Haki za wenye taarifa zitaangaliwa kwa uzito.

  6. Hatua za kimkakati zitachukuliwa ili kuzuia usambazaji wa taarifa za mwanachama bila idhini au kinyume cha sheria. Taarifa zote za mwanachama zinahifadhiwa kwenye kompyuta zenye nywila na zinazotumiwa tu na watu wenye idhini ya kufanya hivyo. Ofisi zenye kompyuta hizo hufungwa baada ya saa za kazi na walioidhinishwa tu ndio wenye ruhusa ya kuingia kwenye ofisi hizo.

  7. Taarifa binafsi hazitatolewa kutoka ofisi moja ya tawi kwenda nyingine ila tu ikiwa ni lazima kufanya hivyo kwa ajili ya kutimiza utendaji wa taasisi au inapohusu michango ya hiari ya taasisi ya SSCF. Wanachama wote wa SSCF wamekubali mambo hayo kwa hiari kwa kujitambulisha na kukubali kuwa wanachama .

Kanuni hizi za kulinda taarifa zinasimamia matumizi ya taarifa za kibinafsi yaliyoonyeshwa kwenye katiba ya chama, ambayo inatolewa kwa wanachama wote wanaofikia hatua ya kuwa wanachama kamili. Kwa habari zaidi, ona katiba ya chama hapa.

Haki ya kulinda taarifa za kila mwanachama na kurekebisha au kufuta taarifa za mwanachama au za siri zinaidhinishwa kulingana na utaratibu wa wanachama uliobainishwa kwenye Katiba.

Sera ya SSCF  ya kulinda taarifa za wanachama iliyobainishwa hapo juu inaonyesha jinsi SSCF inavyoshughulikia taarifa za wanachama wake.

Why People Love Us For Adventures?