VICOBA Vs SACCOS: Ni Kipi Bora?

VICOBA ni kifupi cha maneno Village Community Bank, ikiwa na maana ya Benki ya Jamii ya Watu wa Kijijini.

VICOBA ina historia ndefu ya ufanyaji kazi nchini Tanzania. Dhana ya VICOBA ilianzishwa nchini Tanzania miaka ya 1980 kama njia ya kukabiliana na ukosefu wa huduma za kifedha vijijini. Tangu wakati huo, mtindo huo umekubaliwa na unakuwa kwa kasi nchini, huku maelfu ya vikundi vya VICOBA vikifanya kazi Tanzania nzima.

Katika miaka ya mwanzo ya VICOBA nchini Tanzania, modeli hiyo kwa kiasi kikubwa haikuwa rasmi na inatokana na vyama vya akiba na mikopo (ROSCAs). Hata hivyo, baada ya muda, vikundi vya VICOBA vimeboresha huduma zao, na wengi wamerasimisha shughuli zao na kupata msaada kutoka kwa serikali na mashirika mengine.

Hivi leo, VICOBA ina mchango mkubwa katika kuboresha hali ya kiuchumi ya jamii za vijijini nchini Tanzania, kutoa huduma za kifedha kusaidia ujasiriamali na biashara ndogo ndogo na kukuza elimu na ujuzi wa kifedha.

Licha ya changamoto na mapungufu yalipo, VICOBA inaendelea kuwa sehemu muhimu ya sekta ndogo ya fedha nchini Tanzania, ikisaidia kuleta ujumuishwaji wa kifedha vijijini na kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi.

Wakati huo huo, SACCOS ((Savings and Credit Cooperative Society) ikiwa na maana ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo, ni aina ya taasisi ya kifedha inayomilikiwa na kudhibitiwa na wanachama wake, ambao hutumia huduma zake kuweka na kukopa fedha. Mara nyingi huundwa na vikundi vya watu walio na nasaba moja, kama vile wafanyikazi wa kampuni au wanajamii.

SACCOS inazo faida kadhaa, ikiwa ni pamoja na masharti nafuu ya mikopo, kufikika kwa urahisi, elimu ya fedha, na inadhibitiwa na wanachama wenyewe katika vikao vya maamuzi.

Hata hivyo, SACCOS pia zina madhaifu yake, yakiwa ni pamoja na huduma ndogo, hazisambai kwa haraka kufikia maeneo mengi, upatikanaji wa mtaji wodo, udhibiti mdogo, utaalam mdogo, ukosefu wa ukwasi, na utegemezi kwa watu wa kujitolea.

Kabla ya kujiunga na SACCOS, ni muhimu kufanya utafiti, kuelewa mahitaji ya uanachama, kuangalia sifa, kutathmini huduma, ada na masharti ya mkopo na akiba, kutathmini usimamizi, kusoma sheria ndogo, na kutafuta ushauri ikihitajika.

Kama tulivyoona hapo juu, VICOBA na SACCOS, vyote ni aina ya vyama vya vidogo vya ushirika wa akiba na mikopo vinavyotoa huduma za kifedha kwa wanachama wake.

Hata hivyo, kuna tofauti kadhaa kati ya taasisi hizo mbili:

  1. Uanachama: VICOBA kwa kawaida hupangwa katika ngazi ya kijiji, kata au mtaa, na inaundwa na kikundi kidogo cha wanachama wanaofahamiana, wakati SACCOS huwa ni vyama vikubwa yenye msingi mpana wa wanachama.
  2. Muundo: VICOBA kwa kawaida si rasmi na inafanya kazi kwa kuaminiana na kusaidiana, wakati SACCOS ni rasmi zaidi na ina mfumo wa utawala unaoeleweka na vinadhibitiwa na mamlaka ya kiserikali.
  3. Huduma: VICOBA kwa kawaida huzingatia huduma za kuweka akiba na mikopo, wakati SACCOS mara nyingi hutoa huduma mbalimbali za kifedha, zikiwemo bima na bidhaa za uwekezaji.
  4. Udhibiti: VICOBA huwa havidhibitiwi kama ilivyo kwa SACCOS, ambazo ziko chini ya kanuni na masharti magumu zaidi ya kisheria na udhibiti.
  5. Ufikiwaji: Vikundi vya VICOBA vinaweza kufikiwa zaidi na watu wa vijijini ambao mara nyingi hawawezi kupata huduma za kibenki, wakati SACCOS mara nyingi huwa mijini. Takwimu zinaonyesha kuna idadi ndogo sana zilizoko vijinini ikilinganishwa na maeneo ya mijini

VICOBA na SACCOS zote mbili zina uwezo wa kuboresha upatikanaji wa mitaji na kusaidia maendeleo ya kiuchumi katika jamii ambako zinafanya kazi, na uchaguzi wa ipi bora kati ya moja baina ya nyingine, inatategemena mahitaji ya muhusika au hali maalum ya jamii anakopatikana.

Lusabara

Lusabara

Mwandishi wa makala hii ni mwanafunzi nje ya darasa. Mfikirivu, anayependa kutizama mambo kama yalivyo. Ni teja wa teknolojia na mwanafunzi wa masoko ya kidijitali na usanifu mifumo ya kyomputa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Let's make a difference together

We’re not here to just make a profit, we’re here to create a better world. We’re here to challenge the status quo and disrupt industries. We’re here to empower people and help them achieve their full potential. We’re here to have fun and enjoy the ride. Our mission is to make a positive impact by investing in and supporting innovative and passionate entrepreneurs who share our values. We’re not afraid to take risks and push boundaries, and we believe that by doing so, we can change the world for the better

Recent Posts

Follow Us

Join the thousands on the waitlist and help us reimagine banking for the people.

Grow your audience, chat, follow, like and comment with your friends on the platform. With an ever growing community of hustlers, there’s enough people to connect with and make new friends.